Wali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wali (chakula))
Rukia: urambazaji, tafuta

Kwa Wali kama cheo cha msimamizi wa eneo tazama "liwali"

Wali na kuku kwenye sahani

Wali ni nafaka iliyopikwa kama chakula na hasa mbegu wa mpunga unaoitwa mchele baada ya kazi ya kukoboa yaani kutoa maganda yake.

Neno "wali" hutumiwa pia kwa nafaka za mtama au ngano ikipikwa lakini kwa kawaida watu huelewa wali ya mchele.

Wali ni kati ya vyakula muhimu zaidi duniani. Kama chakula cha watu inashindana kidunia na ngano. Hasa watu wa Asia ya Mashariki na Asia ya Kusini hutegemea wali kama chakula cha kila siku.

Katika Afrika wali ni chakula cha pekee kwa watu wengi isipokuwa pale ambako mpungwa unalimwa. Nje ya hapo wali ni chakula cha sikukuu au cha nafasi ya pekee au ya matajiri. Katika Afrika ya Mashariki chakula kinachopendwa ni kuku na wali au samaki na wali. Chakula cha pekee kabisa ni pilau ambayo ni wali inayochanganywa na viungo maalumu na nyama.

Upishi [hariri]

Kuna njia mbalimbali za kupika wali. Mara nyingi hupikwa katika maji. Wapishi hupima kikombe kimoja cha mpunga na vikombe viwili vya maji na kupika hadi maji yamekwisha basi wali imeiva. Wengine hupendelea kuonja mra kwa mara mpaka wameridhika. Kuna pia sufuria za umeme hasa kwa upishi wa wali.

Katika nchi kama Hispania mpunga kwanza hukaangwa katika mafuta na maji kuongezwa baadaye. Watu wengine wanapendelea kutumia supu badala ya maji kwa kuongeza utamu wa wali.

Aina mbalimbali za mpunga huleta vyakula tofauti. Kuna wali inayotokea laini sana na aina nyingine inatokea imara zaidi.

Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

[[en:Rice}}