Mpunga
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Oryza)
| Mpunga (Oryza spp.) |
||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mpunga wa kiasia
|
||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mpunga ni aina ya mimea katika familia ya manyasi (Poaceae). Spishi kadhaa zinapandwa katika sehemu mbalimbali za dunia, lakini mpunga wa kiasia ni ile ya kawaida.
Mpunga ni chanzo cha chakula kwa watu wengi duniani. Punje (mbegu) zake ni nafaka na huitwa mchele. Mchele uliopikwa ni wali.
Spishi[hariri]
- Oryza barthii, Mpunga-porini wa kiafrika (African wild rice)
- Oryza glaberrima, Mpunga wa kiafrika (African rice)
- Oryza longistaminata, Mpunga stameni-ndefu (Longstamen rice)
- Oryza rufipogon, Mpunga mwekundu (Red rice)
- Oryza sativa, Mpunga wa kiasia (Asian rice)
- Oryza nivara, Mpunga-porini wa kihindi (Indian wild rice)