Savana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Savana katika Mbuga wa Wanyama wa Tarangire, Tanzania
Savana mbele ya mlima wa Oldoinyo Lengai, upande wa Kenya

Savana ni aina ya sura ya nchi penye manyasi na miti michache. Kiasi cha miti kinategemeana na kiasi cha maji au mvua kinachopatikana.

Tabia kuu ya savana ni uhaba wa maji. Tofauti na jangwa maji yapo ingawa ni kidogo. Kiwango cha kawaida ni kati ya milimita 500 na 1500 kwa mwaka.

Savana ina wanyama wa pekee wanaodumu katika mazingira haya. Wengi ni wala majani halafu kuna wala nyama wanaowinda wala majani.

World.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Savana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.