Uvukizaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uvukizaji katika fizikia ni mwendo wa kiowevu (majimaji) kuwa gesi.

Kuna dutu kama maji zinazoanza kuvukiza kabla ya kufikia kiwango cha kuchemka. Viowevu vyote huvukiza vikifikia kiwango chao cha kuchemka.

Kama molekuli katika kiowevu zinapashwa moto mwendo wao unaongezeka. Zinagonganagongana na kuachana mbali zaidi hadi kuwa gesi.

Katika metorolojia uvukizaji ni hasa mwendo wa maji kuwa mvuke au gesi. Mwendo huu ni nguvu muhimu sana katika duara ya maji duniani. Maji ya baharini au unyevu nchini yanapashwa moto hasa na mionzi ya jua hadi kuwa mvuke unaopanda juu kuwa mawingu.

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Uvukizaji" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Uvukizaji kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Vifaa binafsi