Korongo (Bovidae)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Korongo | ||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Dume la korongo
(Hippotragus equinus) |
||||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Korongo au kolongo ni spishi ya kawaida zaidi ya jenasi Hippotragus katika familia Bovidae. Spishi nyingine inaitwa pala hala au mbarapi. Hawa ni wanyama wakubwa ambao wanatokea savana za Afrika zenye miti. Rangi ya madume ni kahawia hadi nyeusi, rangi ya majike ni kahawia. Kuna mabaka meusi na meupe kichwani, lakini hayaonekani sana kwa korongo buluu; tumbo ni jeupe. Dume na jike wana pembe ndefu zilizopindika kuelekea nyuma ambazo urefu wao unaweza kufika mita moja au zaidi lakini fupi zaidi kwa jike. Wanyama hawa hula manyasi marefu kiasi.
Spishi [hariri]
- Hippotragus equinus Korongo (Roan Antelope)
- Hippotragus leucopheus Korongo Buluu (Bluebuck) – imekwisha sasa (k.y. 1800)
- Hippotragus niger Pala Hala au Mbarapi (Sable Antelope)
Picha [hariri]
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Korongo (Bovidae) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.