Ng'ombe
| Ng'ombe | ||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kundi la ng'ombe
|
||||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||
| Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
|
Nususpishi 5:
|
Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. “Ng'ombe-kaya” ni aina zifugwazo za “ng'ombe-mwitu” (Bos primigenius). Kwa asili kuna aina mbili za ng'ombe-kaya: ng'ombe wa Ulaya na ng'ombe wa Uhindi ambazo ni nususpishi za B. primigenius (B. p. taurus na B. p. indicus mtawalia). Zinatoka kwa nususpishi za zamani B. p. primigenius na B. p. namadicus. Sikuhizi ni ngumu kufahamu nususpishi za ng'ombe, kwa sababu takriban aina zote za ng'ombe ni chotara sasa.
Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili. Ng'ombe waliofugwa na binadamu kutokana kwa ng'ombe-mwitu ili kujipatia nyama na maziwa. Katika nchi nyingi hutumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga na kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
Ng'ombe wanapatikana kote duniani na kuna aina kwa kila namna ya hali ya hewa. Wengine huishi katika milima baridi za Uskoti au Skandinavia, wengine katika joto la Afrika au Australia.
Wanacheua chakula chao na huwa na tumbo lenye vyumba vinne. Baada ya kula nyasi mara ya kwanza wanairudisha kutoka chumba cha kwanza cha tumbo na kuitafuna tena. Kwa njia hii wanapata lishe nyingi kutoka nyasi.
Nususpishi [hariri]
- Bos p. africanus Ng'ombe-mwitu wa Afrika imekwisha sasa
- Bos p. indicus Ng'ombe wa Uhindi
- Bos p. namadicus Ng'ombe-mwitu wa Uhindi imekwisha sasa
- Bos p. primigenius Ng'ombe-mwitu imekwisha sasa
- Bos p. taurus Ng'ombe wa Ulaya
Picha [hariri]
-
Mchezo wa ng'ombe hupendwa sana katika nchi zenye utamaduni wa Kihispania
Viungo vya Nje [hariri]
- Cattle Breeds website - Oklahoma State University
- PBS Nature: Holy Cow (about cows in general)
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.