Uskoti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Scotland (Kiingereza)
Alba (Kigaeli)
Uskoti
Bendera ya Uskoti Lionrampant.svg
Bendera Nembo
Wito: Nemo me impune lacessit
(Kilatini: Hakuna anayenichokoza bila adhabu)
Uskoti katika Ulaya


Uskoti katika Ulaya

Uskoti (kijani cheusi) katika kisiwa cha Britania
Uskoti (kijani cheusi) katika kisiwa cha Britania (Uingereza)
Lugha Kiingereza, Kigaeli, Kiskoti
Mji mkuu Edinburgh
Mji mkubwa Glasgow
Waziri Mkuu Alex Salmond
Eneo
- Total
- % water

78,782 km²
1.9%
Wakazi
- Jumla (2001)
- msongamano

5,062,011
64/km²
GDP (PPP)
 • Total
 • Per capita
2002 est.
$130 Billioni
$25,546
Pesa Pound sterling (£) (GBP)
Time zone
 - Summer (DST)
GMT (UTC+0)
BST (UTC+1)
Internet TLD .uk
Calling Code 44

Uskoti ni nchi katika Ulaya. Iko kwa kaskazini ya kisiwa cha Britania Kuu ikiwa ni sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kihistoria Uskoti iliwahi kuwa nchi ya pekee ikaunganishwa chini ya Ufalme wa Uingereza tangu mwaka 1603 BK, tangu 1707 Uskoti haukuwa tena na bunge la pekee lakini ulikuwa na wawakilishi katika bunge la London. Bunge la Uskoti lilirudishwa tena mwaka 1999 linalosimamia mambo ya ndani.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Uskoti ni theluthi ya kaskazini ya kisiwa cha Britania. Eneo lake ni 78,772 km². Upande wa kusini Uskoti imepakana na Uingereza mwenyewe. Upande wa mashariki kuna Bahari ya Kaskazini, upande wa kazkazini na magharibi Atlantiki pamoja na bahari ya Eire.

Pamoja na bara Uskoti ina visiwa 790.

Ndani ya nchi kuna kanda tatu:

  • Nyanda za Juu
  • tambarare za chini
  • vilima vya Kusini

Mlima mkubwa wa Uskoti ni Mlima Nevis karibu na Fort William mwenye kimo cha 1,344 m.

Upande wa magharibi wa Uskoti bara iko funguvisiwa ya Hebridi. Upande wa kaskazini kuna visiwa vya Orkney na vya Shetland.

Miji kumi mikubwa ya Uskoti[hariri | hariri chanzo]

Mji Wakazi
5 Aprili 1991
Wakazi
29 Aprili 2001
Glasgow (Glaschu) 658.379 629.501
Edinburgh (Dùn Èideann) 400.632 430.082
Aberdeen (Obar Dhèathain) 182.133 184.788
Dundee (Dùn Dè, Dùn Dèagh) 157.808 154.674
Paisley (Paislig) 73.925 74.170
East Kilbride (Cille Bhrìghde an Ear) 70.579 73.796
Hamilton (Hamaltan) 49.988 48.546
Cumbernauld (Comainn nan Allt) 49.507 49.664
Greenock (Grianaig) 49.267 45.467
Ayr (Àir) 47.962 46.431

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Picha za Uskoti[hariri | hariri chanzo]