Hali ya hewa
Hali ya hewa (pia: halihewa) ni namna ya kutaja yale yanayotokea katika sehemu ya chini ya angahewa juu ya uso wa dunia katika eneo fulani na wakati fulani.
Hali hizi hutofautishwa kulingana na upepo, halijoto, mawingu, unyevuanga, kanieneo, mnururisho wa jua, uvukizaji na kadhalika.
Athari muhimu zaidi katika mabadiliko ya halihewa ni mzunguko wa angahewa unaotawaliwa na nishati ya mnururisho wa jua na uwiano wa kanieneo katika sehemu mbalimbali za angahewa.
Tabia muhimu za halihewa hutokea kama upepo, dhoruba, kimbunga, radi, mvua, theluji na baridi au joto zikiathiri maisha ya binadamu.
Hali ya hewa inaenda sambamba na tabianchi yaani, kama ni ya joto au baridi, bichi au yabisi. Mabadiliko ya hali ya hewa hurahisisha maisha au kuongeza ugumu wake, hasa kama mabadiliko yanavuruga kukua kwa mimea kwa njia ya ukame au mafuriko.
Watu hujenga makao na kuvaa nguo kulingana na halihewa na kwa njia hiyo tabianchi imekuwa nguvu ya kufinyanga utamaduni wa watu.
Meterolojia kama elimu ya hali ya hewa
[hariri | hariri chanzo]Sayansi ya metorolojia huifanyia halihewa utafiti kwa kupima hali mbalimbali hadi kutabiri mabadiliko yanayokuja karibuni.
Sayansi hii inafundishwa kwenye vyuo vikuu na siku hizi kila nchi huwa na idara ya serikali inayoangalia hali ya hewa, kwa mfano Idara ya Metorolojia Kenya au Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Hali ya hewa na utamaduni
[hariri | hariri chanzo]Hali ya hewa hutazamwa tofauti katika tamaduni na nchi mbalimbali. Katika Afrika penye hatari ya ukame kwa kawaida mvua hutazamwa kama baraka; lakini Ulaya penye mvua nyingi watu hufurahia jua na watoto wanaweza wakaambiwa: "Usipomaliza chakula kwenye sahani yako mvua itanyesha" (msemo wa Kijerumani).
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Internet Geography's weather page Ilihifadhiwa 24 Machi 2008 kwenye Wayback Machine.
- The Weather Channel
- Kenya Meteorological Department
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hali ya hewa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |