Unyevuanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Unyevu anga ni kiwango cha mvuke wa maji katika angahewa kwa jumla, katika hewa ya eneo fulani au ndani ya majengo.

Unyevu anga ni kipimo muhimu kwa ajili ya michakato mingi ya hali hewa, teknolojia na afya ya watu, wanyama au mimea.

Vipimo vya unyevuanga[hariri | hariri chanzo]

Hewa inaweza kushika ndani yake kiasi fulani cha mvuke kutegemeana na halijoto yake. Unyevu anga hupimwa kwa asilimia; kipimo hiki kinataja uwiano kati ya mvuke uliopo wakati huu na kiwango cha mvuke kinachowezekana kwenye halijoto fulani, maana ni tofauti kiasi kati ya Dar es Salaam na Nairobi.

Jedwali linalofuata linaonyesha unyevuanga wa juu kwenye halijoto fulani; kanieneo ni ile ya uwiano wa bahari au mahali pa pwani. Unyevuanga wa juu huwa tofauti mlimani ambako kanieneo angahewa imepungua.

Halijoto 10 °C 12 °C 14 °C 16 °C 18 °C 20 °C 22 °C 24 °C 26 °C 28 °C
Unyevuanga wa Juu 9.4 g/ 10.6 g/m³ 12 g/m³ 13.6 g/m³ 15.3 g/m³ 17.2 g/m³ 19.3 g/m³ 21.7 g/m³ 24.3 g/m³ 27.1 g/m³

Maana yake ni kwamba mita moja ya ujazo inaweza kushika hadi gramu 12 ya maji (kwa umbo la mvuke) ndani yake kama halijoto ya hewa ni sentigredi 14. Lakini kama halijoto ni 26 °C mita ya ujazo unaweza kushika hadi gramu 21.7. Viwango hivi ni unyevuanga wa juu unaowezekana.

Kama unaongezeka -kwa mfano kwa kuchemsha maji chumbani - tunaona utoneshaji wa mvuke yaani kutokea kwa ukungu au matone ya maji; mvuke unaowevyeka kuwa maji tena - si mvuke wote hewani lakini kiasi kinachozidi uwezo wa hewa kulingana na halijoto.

Kama kuna halijoto ya 26 °C na kiasi cha mvuke ni gramu 11 kwa kila tunasema unyevu anga ni asilimia 50.

Mfano[hariri | hariri chanzo]

Tukipika maji nyumbani wakati wa miezi ya baridi tunaona mvuke sentimita chache juu ya sufuria tu lakini hatuioni katika hewa ya chumba. Lakini baada ya muda kidogo matone yanaonekana kwenye kioo cha dirisha - hapa maji yanawevyeka na kutonesha hapa.

Kutokana na baridi nje hewa karibu na kioo cha dirisha ni baridi zaidi haiwezi kushika kiwango cha unyevu kama hewa la joto zaidi chumbani, hivyo kutonesha kwa maji.

Katika gari machakato huu unaweza kuleta hatari kama madirisha yanafunikwa kwa matone na dereva hawezi kuona tena yanayotokea nje. Hapa magari huwa na mitambo ya kupuliza hewa joto zaidi juu ya uso wa dirisha na kusababisha matone ya maji kupotea kwa uvukizaji.