Mafuriko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mafuriko katika eneo la TAZARA, Dar es Salaam, Tanzania
Mafuriko ya mto Elbe mjini Dresden, Ujerumani
Mafuriko huko Jangwani mjini Dar es Salaam, Tanzania

Mafuriko ni hali ya kuwa na maji mengi yanayofunika nchi kavu pasipo na maji kwa kawaida.

Mafuriko yanaweza utokea

  • popote baada ya mvua mkali unaoteremsha maji mengi yasiyo na njia ya kupotea hasa baada ya kutelemka penye mlima au mtelemko
  • kando la mto ama baada ya mvua mkali au wakati wa mvua nyingi au kwenye majira ya kuyeyuka kwa theluji
  • kando la ziwa au bahari kama upepo mkali unasukuma maji kuelekea pwani hasa pamoja na kutokea kwa kwa maji kujaa au bamvua

Mafuriko mara nyingi ni hatari kwa binadamu huleta hatari kwa maisha, mali na nyumba. Njia za kujiokoa ni pamoja na kuhama haraka penye miinuko au nchi ya juu zaidi; watu waliozoea mafuriko wana mbinu za pekee kama vile kujenga vizuizi vya maji kupanda juu, kuchimba mifereji inayopeleka maji mabli au kujenga nyumba juu ya vilima wakijua hakuna njia ya kuzuia mafuriko.

Maafa kutokana na mafuriko[hariri | hariri chanzo]

Hapo ni orodha ya mafuriko yanayojulikana kuleta maafa mengi.

Idadi ya vifo Tokeo Mahali Mwaka
2,500,000–3,700,000[1] Mafuriko ya China 1931 China 1931
900,000–2,000,000 Mafuriko ya Hwangho 1887 China 1887
500,000–700,000 Mafuriko ya Hwangho 1938 China 1938
231,000 Kuvunjika kwa mlambo wa Banqiao; takriban watu 86,000 walikufa kutokana na mafuriko na wengine 145,000 kutokana na magonjwa yaliyofuata China 1975
230,000 Tsunami kwenye Bahari Hindi 2004 Indonesia, Uhindi, Sri Lanka 2004
145,000 Mafuriko ya Yangtze 1935 China 1935
zaidi ya watu 100,000 Mafuriko ya Uholanzi 1530 Netherlands 1530
Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mafuriko kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.