Tsunami

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Watu walikimbia wimbi la tsunami tar. 26 Desemba 2004 lilipogonga mwambao wa Ao Nang nchini Uthai
Uenezaji wa mawimbi ya tsunami wa Krismasi 2004 katika Bara Hindi

Tsunami ni wimbi kubwa sana katika bahari inayosababishwa na tetemeko la ardhi, mlipuko wa volkano au matokeo mengine yanayosababisha mshtuko wa ghafla chini ya maji. Mshtuko huu unasababisha kutokea kwa wimbi kali linaloanza kupaa juu likifika katika maji kame.

Neno tsunami linatokana na lugha ya Kijapani likimaanisha bandari ya mawimbi.

Tsunami huweza kutokea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Wakati mwingine inaweza kutokea bila kuleta madhara yoyote.

Tsunami wa Krismasi 2004[hariri | hariri chanzo]

Tar. 26 Desemba 2004 lilitokea tetemeko la ardhi chini ya Bahari Hindi karibu na pembe ya kaskazini ya Sumatra kwenye mstari ambako bamba la Uhindi linajisukuma chini ya bamba ndogo la Burma. Siku ile 1,200 km za pembizo la bamba la Uhindi zilisogea mbele katika muda wa dakika chache kwa urefu wa takriban 15 m chini ya bamba la Burma. Bamba la juu lilisukumwa na kupaa juu hadi mita 30. Mshtuko huu ulianzisha wimbi kubwa chini ya bahari lililotokea juu kwa umbo la tsunami lililoua takriban watu 275,000.

Katika maji marefu ya bahari wimbi halikuwa na hasara likaonekana kuwa na 30 cm pekee. Lakini ilifika mwambaoni kwenye maji kama likaanza kupaa juu kufikia hadi 30 m.

Kutoka kitovu cha tetemeko la ardhi mawimbi ya tsunami yalienea kote. Yalipiga vikali sana pwani za Indonesia, Sri Lanka, Thailand na India. Mawimbi yalifikia hadi pwani la Afrika na kusababisha vifo katika Somalia, Kenya, Tanzania na Afrika Kusini.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]


Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tsunami kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.