Bakteria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bakteria jinsi zinavyoonekana chini ya hadubini
Bakteria ya Escherichia coli ziliongezwa ukubwa mara 25,000

Bakteria (Kigir. βακτήριον baktērion „kijiti“) vi viumbe vodogo sana aina ya vidubini. Huonekana kwa hadubini tu na kwa sababu hiyo hazikujulikana kwa karne nyingi.

Mwili wa bakteria huwa na seli moja tu. Kuna aina nyingi sana na idadi ya bakteria ni kubwa kushinda viumbe vyote vingine duniani.

Huishi kwenye ardhi na kwenye maji ziko pia hewani zinaposukumwa na upepo. Aina nyingi huishi ndani ya viumbe vikubwa zaidi. Mwanadamu huwa na bakteria nyingi ndani ya utumbo wake ambazo ni lazima kwa kumeng'enyuka kwa chakula ndani yetu. Lakini bakteria za nje ya mwili huweza kusababisha magonjwa na sehemu kubwa ya magonjwa ya kuambukizwa yametokana na bakteria.

Bakteria huzaa kwa njia ya kujigawa na kuwa bakteria mbili ambazo ni sawa na seli asilia.

Bakteria ya kawaida huwa na kipenyo cha 1 µm (mikromita 1).

Tazama pia [hariri]

Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bakteria kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.