Okapi
| Okapi | ||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Okapi
|
||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Okapi (Okapia johnstoni) ni mamalia wa familia ya twiga. Umbo lake hufanana na farasi ina michoro miguuni kama punda milia lakini haina uhusiano naye ni aina ya twiga.
Okapi ni mnyama aliyejulikana na wenyeji wa maeneo yao tu hadi mwaka 1901. Hapo zamani ilikuwa inaaminika kuwa mnyama huyu hupatikana tu katika misitu ya Ituri lakini mwaka 2006 zilipatikana dalili zilizoonyesha kwamba mnyama huyu yuko pia kwenye misitu ya hifadhi ya kitaifa ya Kongo ya Virunga. Kwenye misitu ya Ituri kuna hifadhi ya okapi yenye eneo la 14,000 km².
Shingo yake ni fupi kuliko twiga lakini ina ulimi mrefu sana wa kujipatia majani unaomwezesha kusafisha masikio yake yeye mwenyewe. Duma ina pembe mbili fupi kichwani.
Ukubwa wa okapi ni hadi 2.5 m kichwani na hadi 2 m mabegani. Anafikia uzito kati ya kg 200 hadi 250. Anakula majani ya miti pamoja na manyasi, matunda na uyoga.
Viungo vya nje [hariri]
Picha [hariri]
-
Okapi kwenye bustani ya wanyama ya Bristol (Uingereza)
-
Okapi wa dume akionyesha ulimi kwenye bustani ya wanyama ya Bristol (Uingereza)
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.