Punda milia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Punda milia
Punda milia
Punda milia
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Perissodactyla(Wanyama wenye kidole kimoja au vitatu mguuni)
Familia: Equidae (Wanyama walio na mnasaba na farasi)
Jenasi: Equus
Linnaeus, 1758
Spishi: E. grevyi Oustalet, 1882

E. quagga Boddaert, 1785
E. zebra Linnaeus, 1758

Punda milia

Utangulizi[hariri | hariri chanzo]

Punda milia ni wanyama wa familia ya ‘equids’ wa Afrika wanafahamika sana kwa rangi yao ya pekee ya michirizi myeupe na myeusi, michirizi yao huwa na mpangilio tofauti kwa kila pundamilia mmoja. Ni wanyama wenye kuchangamana sana na huonekana mara nyingi huonekana kwenye makundi madogo na hata makubwa. Mbali na michirizi yao,pundamilia wana nywele shingoni tofauti na ndugu zao wa kambo, farasi, na punda. Punda milia hajawahi kufungwa kwa mafanikio. Kuna spishi tatu za pundamilia, Plains Zebra, Grévy's Zebra na Mountain Zebra. Plain zebra na Mountain Zebra wapo kwenye jenasi ndogo ya ‘Hippotigris’ lakini Grevy’s zebra akiwa kwenye Delichohippus huyu wa mwisho anafanana na punda huku wale wawili wa mwanzo wakifanana na farasi. Hata hivyo,chembe asili na data za molekyuli zinaonesha kuwa pundamilia hasa wana asili ya “monophyletic” Wote watatu wako kwenye jenas ya ‘Equus’ pamoja na wanafamiia wa ‘Equids’. Katika maeneo fulani ya huko Kenya, Plains Zebra na Gorevy’s zebra wapo pamoja.

Upekee wa michirizi na tabia za pundamilia inawafanya kuwa miongoni mwa wanyama wanaofahamika sana kwa binadamu. Punda milia hupatikana katika maeneo mbalimbali,kama vile ukanda wa mbuga, savanna, ukanda wa misitu,kwenye vichaka vya miiba,milimani na kwenye vilima vya pwani.hata hivyo sababu mbalimbali za muingiliano wa jamii na tamaduni huleta athari kubwa katika idadi ya pundamilia, hasa kutafuta ngozi na uharibifu wa makazi. Grevy’s Zebra na Mountain Zebra’ wapo hatarini kutoweka. Huku Plain Zebra wakizidi kuwa wengi, spishi moja,’ quagga’ilitoweka kabisa mwishoni mwa karne ya 19. Jina la ‘zebra’ limetokana na neno la Kireno cha zamani, lisemalo ‘zeura’ likimaanisha punda wa porini.


Uanishaji na mabadiliko[hariri | hariri chanzo]

Punda milia walikuwa ni wa ukoo wa pili kutoka kwa ‘farasi wa mwanzo’, baada ya punda, kama takribani miaka milioni 4 iliyopita. Grevy’s Zebra huaminika kuwa ndio aina ya pundamilia ya kale zaidi na yakwanza kutokea.wanyama wa kwanza jinas ya ‘Equus’ inaaminika kuwa walikuwa na michirizi na hivyo zebra wamedumu na mistari hiyo mpaka sasa kutokana na kuchangamana kwao hasa katika sehemu za tropic. Michirizi itakuwa haina kazi yeyote /faida kwa wanyama familia ya equids wanaishi kwa uchache sehemu za jangwani (kama vile punda na baadhi ya farasi) na kwa wale wanaoishi kwenye maeneo yenye baridi na kupukutisha kila mwaka (kama baadhi ya farasi) [1] mabaki ya ‘equids’ wa kale zaidi yaligunduliwa huko Hagerman Fossil Beds National Monument; Hagerman, Idaho. Kisha yaliitwa Hagerman horse’ na jina la kisayansi Equus simplicidens’. Inaaminika kuwa walikuwa sawa na Grevy’s zebra [2] wanyama hawa walikuwa na maumbo mafupi na yakujaa kama pundamilia na fuvu la kichwa jembamba kama la punda. [3] Gravy’s Zebra pia walikuwa na fuvu la kichwa mithili ya lile la punda. Hagerman horse pia huitwa pundamilia wa Amerika au pundamilia wa Hagerman.


Uanishaji[hariri | hariri chanzo]

Punda milia huko Botswana.

Kuna spishi tatu ambao wanaeleweka vizuri; kwa pamoja spishi mbili hapa wanajumla ya nususpishi nane. Punda milia ndio waliotawanyika zaidi,na mahusiano kati yao na baadhi ya nususpishi nyingine hazijaeleweka vizuri.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Nusujenasi: Hippotigris

Nusujenasi: Dolichohippus


[1] Punda milia zeruzeru akifugwa


Punda milia wa kwenye nyanda ‘Plains Zebra’ (Equus quagga) ndogo takribani kumi na mbili waliosambaa sehemu kubwa za kusini mashariki mwa afrika.ingawa pundamilia wanajamii nyingi zenye kufanana, lakini hawachanganyani katika kuzaliana kila spishi huweza kuzaa tu kwa uwezo wao mpaka tu kwa msaada wa sayansi.


Maumbile ya punda milia na matumizi yake.[hariri | hariri chanzo]

Michirizi[hariri | hariri chanzo]

Iliaminika hapo awali kuwa punda milia walikuwa kwanza na rangi nyeupe ndipo mistari ikatokea, sababu tu wanasehemu nyeupe ya chini ya tumbo,hata hivyo utafiti katika ukuaji hasa hatua nyakati za kijusi,imeonekana kuwa mnyama huyu ana rangi nyeusi na michirizi myeupe kuja baadae kama nyongeza pamoja na viwele[2]


camouflage.jpg Punda milia mama akimlea akiwa na mwanae kichakani


Michirizi ya wima huwa kichwani, shingoni na sehemu kubwa ya mwili wake,huku michirizi ya ulalo ikiwa hasa maeneo ya nyuma na miguuni. Alama za punda milia za barabarani ziliitwa hivyo kutokana na michirizi hii ya punda milia. Hufikiriwa kuwa michirizi hii hutumiwa kwa utambuzi baina yao. [3] Kwa kuwa na mtindo tofauti wa michirizi kwa kila punda milia basi wao huweza kutambuana kwa michirizi hiyo. Wengine huamini kuwa michirizi hii ni kwa ajili ya kumsaidia kujificha na kujihami na mazingira yao. Hii huwa kwa namna mbalimbali. Michirizi ya wima huwasaidia punda milia kujificha kwenye nyasi, na huwa na manufaa makubwa hasa kujificha ili simba wasiwaone, sababu simba hawatambui rangi. Kwa kawaida punda milia aliyesimama kwenye nyasi ndefu hawezi kuonwa kabisa na simba.Pia kwa wanyama wafananao kama pundamilia hukaa pamoja na hutembea pamoja.[4] Michirizi husaidia kuwachanganya wanyama wanaowawinda na kufanya vigumu kwa wao kuwakamata.pindi waanzapo kukimbia huelekea pande tofauti ili kuendelea kuwachanganya zaidi washambuliaji washidwe kumchagua pundamilia mmoja na kufanikiwa kumkamata; japokuwa wanabaiolojia hawajaona bado simba anapochanganywa na punda milia


rownikowa Equus burchelli boehmi RB3.jpg Punda milia akitembea

Mwendo[hariri | hariri chanzo]

Kama farasi punda mila hutembea, huenda kwa mwendo wa shoti na kukimbia kwa kawaida huwa na mwendo wa taratibu na stamina yao sana ndio huwasaidia kuwashinda adui zao. Wanapofukuzwa punda milia huenda kwa mwendo wa zi-zag kila upande kumpumbaza mwindaji. Adui anapokaribia, punda milia humshambulia adui kwa nyuma,na kupiga teke au kumngata adui.


portrait.jpg Punda milia kwa karibu

Milango ya fahamu[hariri | hariri chanzo]

Punda milia wana uono mzuri, inafahamika kuwa wanaona kwa rangi pia macho yao yapo kwa pembeni huwapa uwanja mkubwa wa kuona. Punda milia pia huona nyakati za usiku japo si kama adui zao wanao wawinda lakini kusikia kwao vyema ni fidia.

Punda milia husikia vizuri sana na masikio yao ni ya duara zaidi kuliko ya farasi kama ilivyo kwa farasi, punda milia wanaweza kuzungusha masikio yao upande wowote. Zaidi ya hayo, punda milia wanauwezo mzuri wa kunusa na kuonja.


Ikolojia na tabia[hariri | hariri chanzo]

Makundi ya twiga[hariri | hariri chanzo]

Animals.jpg Punda milia katika Tanzania

Kama ilivyo kwa familia ya farasi, punda milia pia huchangamana na jamii zao pia hutegemea na spishi husika. Punda milia wa mlimani na nyikani huishi kwenye makundi wenye dume mmoja na walau majike site na watoto wao. Madume ambao hawana familia huishi kila mmoja peke yake kwenye makundi makubwa ya madume wasio na familia mpaka pale watakapo weza kutafuta jike kwa ajili ya kuanzisha familia, wanapovamiwa na fisi na mbwa mwitu punda milia hujikusanya pamoja na watoto katikati huku wakijitahidi kuwafukuza adui. Kama farasi wengine punda milia hulala (husinzia) huku wamesimama na hulala wakati majirani wakiwalinda na maadui.


Mawasiliano[hariri | hariri chanzo]

eating.JPG Punda milia akila nyasi

Punda milia huwasiliana kwa kubweka kwa sauti kubwa na kulialia, masikio ya punda milia huonyesha namna anavyojisikia. Akiwa kwenye hali ya utulivu na kirafiki masikio yake husimama anapoogopeshwa, masikio yake husimama anapokuwa na hasira, masikio yanarudi nyuma. Anapokuwa anaangalia adui husimama kwenye usimamo wa utayari masikio yamesimama kichwa kipo huku akiangalia, hisia zinapozidi hususani anapomuona adui punda milia hubweka kwa sauti.


Dallas Zoo 1974.jpg Mama na ndama katika Dallas Zoo

Chakula na malisho[hariri | hariri chanzo]

Punda milia ni wanyama wala nyasi wanaozoea mazingira mbalimbali.Hula hasa kwenye nyasi lakini pia hula majani ya miti, mashina mizizi na magamba ya miti Mfumo wao wa mmeng'enyo wa chakula huwawezesha kula chakula imara hata chenye virutubisho kidogo na kuishi.

Uzazi[hariri | hariri chanzo]

Kama ilivyo kwa wanyama wengi, pundamilia jike hukua haraka kuliko punda milia dume. Jike huweza kupata mtoto akiwa na miaka mitatu tu wakati kwa dume ni mpaka miaka mitano au sita. Jike huweza kupata mtoto kila baada ya miezi kumi na mbili na hukaa na mtoto kwa takribani mwaka mmoja. Kama ilivyo kwa farasi, ndama wa punda milia huweza kusimama kutembea na kunyonya muda mfupi tu kisha kuzaliwa. Wanapozaliwa ndama wa pundamilia huwa na rangi ya kahawia na nyeupe badala ya nyeusi na nyeupe. Ndama na punda milia wa mlimani na wale wa nyikani hutunzwa na mama zao na baba zao pia.

Mwingiliano na binadamu[hariri | hariri chanzo]

[5] Lord Rothschild akiwa na punda milia wakikokota kmokoteni (Equus burchelli), ambao alienda nao London mara kadhaa.

Ufugwaji[hariri | hariri chanzo]

Majaribio kadhaa yalifanywa kujaribu kumtumia punda milia kukokota mkokoteni kwa sababu ya ustahimilivu wake wa magojwa kuliko farasi, hata hivyo mengi ya majaribio haya yalishindikana kutokana na tabia za asili za punda milia kucharuka pindi anapobugudhiwa.

[6] Punda milia aliyefugwa akiendeshwa katika Afrika Mashariki.

Captain Horace Hayes, katika “Points of the Horse” (circa 1893) aliainisha matumizi ya aina mbalimbali za punda milia. Huyu bwana alitumia pundamilia wa milimani na kumuendesha kwa siku mbili na punda milia alimudu pamoja na mkewe na kupiga nae picha. Aligundua kuwa punda milia wa aina ‘Burchell’ ni rahisi kuwatumia na ndio chaguo sahihi hasa kwa kufuga sababu walikuwa na kinga ya kun’gatwa na mbung’o. Pia pia alionelea wengine waitwao ‘quagga’ wanafaa vilevile kwa sababu ilikuwa rahisi kuwafundisha kuwapanda na kuvuna.


Uhifadhi[hariri | hariri chanzo]

Binadamu leo anaathari kubwa sana kwa punda milia. Punda milia mpaka sasa bado wanawindwa sana kwa ajili ya ngozi ya zao, Huko Afrika ya Kusini punda milia waliwindwa na kufikia kiasi cha pungufu ya 100 mnamo mwa 1930; hata hivyo sasa wameongezeka na kufikia 700 kutokana na juhudi za utunzaji. Curtural depictions Punda milia wamehusishwa na hadithi za kale za Afrika zinazoelezea ni kwa namna gani walipata mistari ya myeusi kutokana na hadithi ya Bushmen ya huko Namibia, punda milia hapo awali alikuwa anarangi nyeupe lakini alipata mistari myeusi baada ya kupigana na nyani kwenye tundu la maji. Baada ya kumpiga nyani mara kadhaa, punda milia alikosa stamina na kuangukia fimbo/ vijiti vilivyokuwa vinawaka moto vilivyo muunguza na kuacha makovu juu ya ngozi yake nyeupe . Kwenye filamu ya Fantasia, kentaro wawili walioneshwa kama nusu punda milia na nusu mwanadamu badala ya nusu farasi na nusu binadamu kama ilivyo zoeleka.


[7] Mchoro wa pundamilia uliochorwa na Ludolphus

Pundamilia ni kiungo muhimu kwenye sanaa. Kiongozi wa Mughall, jJahangir (v.1605-24) alidhihirisha mchoro wa pundamilia uliochorwa naUstad Mansur. Michirizi ya pundamilia pia ni maarufu kwenye fanicha, mazulia, na mitindo.

Kwenye filamu na katuni, punda milia huwa washriki wa kawaida, lakini huwa na uongozi Fulani mfanoMadagascar and Racing Stripes Punda milia pia hutumika kama alama ya bidhaa na mashirika, kama vileZebra Technologies and Fruit Stripe. Pia punda milia wanaonekana kwenye taifa ya Botswana.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]