Punda
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Punda | ||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Punda-kaya katika Hifadhi ya Taifa ya Amboseli
|
||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| Ngazi za chini | ||||||||||||||
|
Spishi 4: |
Punda ni wanyama wakubwa kiasi wa nusujenasi Asinus ya jenasi Equus katika familia Equidae. Wanafanana na farasi mdogo. Punda anayejulikana sana ni yule anayefugwa, lakini kuna punda porini pia. Watu humtumia punda afugwaye kwa kubeba mizigo, kuvuta magari au kumrakibu. Punda wanaweza kuzaliana na farasi lakini watoto wao hawazai tena kwa kawaida.
Spishi [hariri]
- Equus africanus, Punda wa Afrika (African Wild Ass)
- Equus a. africanus, Punda Nubi (Nubian Wild Ass)
- Equus a. somalicus, Punda Somali Somali Wild Ass)
- †Equus a. atlanticus, Punda Kaskazi Atlas Wild Ass – imekwisha sasa
- Equus asinus, Punda-kaya (Donkey) – huhesabika mara nyingi kama nususpishi ya E. africanus
- Equus hemionus, Punda wa Asia (Onager au Asiatic Ass)
- Equus h. hemionus, Punda wa Mongolia (Mongolian Wild Ass, Khulan au Kulan)
- Equus h. khur, Punda wa Uhindi (Indian Wild Ass au Khur)
- †Equus h. hemippus, Punda wa Syria (Syrian Wild Ass) – imekwisha sasa
- Equus h. kulan, Punda wa Turkmenistan (Turkmenian Kulan)
- Equus h. Luteus, Punda wa Gobi (Gobi Kulan au Dziggetai)
- Equus kiang, Kiang' Kiang)
- Equus k. kiang, Kiang' Magharibi (Western Kiang)
- Equus k. holdereri, Kiang' Mashariki (Eastern Kiang)
- Equus k. polyodon, Kiang' Kusi (Southern Kiang)
- Equus k. chu, Kiang' Kaskazi (Northern Kiang)
Spishi za kabla ya historia [hariri]
- Equus calobatus, Punda Miguu-mirefu (Stilt-legged Onager)
- Equus cumminsii, Punda wa Cummin (Cummin’s Ass)
- Equus francisci, Punda Kibete (Pygmy Onager)
- Equus hydruntinus, Punda wa Ulaya (European Ass)
- Equus lambei, Punda wa Yukon (Yukon Wild Ass)