Reli ya garimoshi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Reli za garimoshi)
Makala hiyo kuhusu "Reli ya garimoshi" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Reli ya garimoshi pamoja na kiti chake

Reli za garimoshi ni nondo au pau za feleji zenye umbo maalumu. Zinalazwa mbili-mbili juu ya boriti imara na kuunda njia ya reli ambako treni zinatembea.

Zamani kulikuwa pia na reli hizi za ubao, baadaye chuma udongo au chuma mfuo. Reli za kisasa hutengezewa kwa feleji pekee zinazotengenezwa kiwandani kuwa na umbopande maalumu.

Umbopande wa reli ya garimoshi

Umbopande wa reli huwa na sehemu tatu ambazo ni

  • kichwa
  • katikati
  • mguu.

Kichwa ni pana na ubora wake unasababisha mwendo barabara ya treni juu reli. Katikati ni nyembamba kwa kusudi la kupunza uzito na gharama. Mguu unaweza kuwa pana au nyembamba zaidi na hii inategemea aina ya kiti kinachobeba reli yenyewe juu ya boriti za chini. Kila kampuni ya reli inatumia maumbo yaliyosanifishwa kwa eneo lake.

Kwa usafiri wa kisasa reli ni lazima kutengenezwa kwa kutumia feleji bora maana inapaswa kubeba mzigo mkubwa mara nyingi kila siku. Feleji ianyofaa kwa ujenzi haufai tena kwa reli za garimoshi maana ilichoka mapema na kuvunjika ni hatari kwa maisha ya abiria na gharama kubwa kwa kampuni ya reli na umma.

Kwa jumla inawezekana kusema kiasi reli hizi ni nzito pamoja na boriti na msingi chini ya boriti ni pia treni nzito na haraka zaidi zinazoweza kuzitumia.

Picha za reli ya garimoshi[hariri | hariri chanzo]

(gusa picha kwa puko kwa maelezo)