Ulaya ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Ulaya ya Mashariki ni sehemu ya mashariki ya bara la Ulaya lakini hakuna uelewano juu ya mipaka yake hasa upande wa magharibi.

Ulaya ya Mashariki kufuatana na Umoja wa Mataifa [hariri]

Umoja wa Mataifa hujumuisha nchi zifuatazo humo:

Orodha hii imejumlisha nchi zote za Ulaya zilizokuwa sehemu za Umoja wa Kisovyeti au zilizoshikamana nao kisiasa hadi 1989 (isipokuwa Ujerumani ya Mashariki). Tatizo lake ni ya kwamba watu wa Poland, Hungaria Uceki na Slovakia zinajihesabu kuwa sehemu za Ulaya ya Kati.

Ulaya ya Mashariki kijiografia [hariri]

Kijiografia mara zinatajwa humo nyingi nchi za Ukraine, Belarus, Moldova na upande wa Ulaya wa Urusi. Isipokuwa sehemu za kaskazini za Urusi huhesabiwa mara nyingi upande wa Ulaya ya Kaskazini.

Ulaya ya Mashariki kiutamaduni [hariri]

Mara nyingi nchi zinazokaliwa na watu wenye lugha za Kislavoni huhesabiwa humo. Lakini kwa njia hii Romania na Hungaria si nchi za Ulaya ya Mashariki lakini Uceki, Slovenia na Kroatia zimo. Kihistoria hata sehemu za Ujerumani zilikaliwa na Waslavoni na Wasorbi katika mashariki bado hutumia lugha yao.

Hivyo kuna nji ya pili inayosema: Nchi zote zenye lugha za Kislavoni zilizoguswa hasa na kanisa orthodoksi kama vile Urusi, Ukraine, Belarus.