Mwinjili Luka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Luka akimchora kwa mara ya kwanza Bikira Maria, kielelezo cha imani katika Injili yake.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Mwinjili Luka (kwa Kigiriki Λουκᾶς, Lukas) ni Mkristo wa karne ya 1 ambaye tangu zamani za Mababu wa Kanisa anasadikiwa kuwa mwandishi wa Injili ndefu kuliko zote za Biblia ya Kikristo.

Vilevile anasadikiwa kuwa mwandishi wa kitabu cha Matendo ya Mitume kinachoendeleza Injili hiyo ili kuonyesha kazi ya Yesu Kristo ilivyoendelea katika Kanisa lake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Hivyo Luka, mwandishi pekee wa Agano Jipya asiye Myahudi, anahesabiwa kuwa ameandika robo ya sehemu hiyo ya pili ya Biblia nzima ya Ukristo.

Pamoja na Wakristo wengine wengi, Kanisa Katoliki linamheshimu kama mtakatifu na msimamizi wa madaktari hasa katika sikukuu yake, tarehe 18 Oktoba[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Luka alizaliwa katika familia ya Kiyunani, labda mjini Antiokia ya Syria, leo nchini Uturuki.

Inasadikiwa aliongozwa na Mtume Paulo kumpokea Yesu na alifanya naye kazi kwa takribani miaka 18. Pamoja na ukaribu huo, hata hivyo hakuandika mitazamo ya Paulo, hii ni kuonesha kuwa aliyaandika yale aliyovuviwa na Roho Mtakatifu.

Anatajwa na Paulo katika barua zake kama mganga aliye jirani naye katika majaribu yake: Waraka kwa Filemoni, mstari 24; Waraka kwa Wakolosai 4:14 na Waraka wa pili kwa Timotheo 4:11.

Uaminifu huo wa Luka kwa Paulo unalingana na habari za Matendo ya Mitume, ambapo Luka hajitaji, lakini anasimulia safari za Paulo akitumia mara nyingi neno "sisi". Hivyo anajishuhudia kuwa mshiriki wa utume wake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • I. Howard Marshall. Luke: Historian and Theologian. Downers Grove, Illinois: InterVarsity Press.
  • F.F. Bruce, The Speeches in the Acts of the Apostles. London: The Tyndale Press, 1942.[1] Archived 31 Mei 2012 at the Wayback Machine.
  • Helmut Koester. Ancient Christian Gospels. Harrisburg, Pennsylvania: Trinity Press International, 1999.
  • Burton L. Mack. Who Wrote the New Testament?: The Making of the Christian Myth. San Francisco, California: HarperCollins, 1996.
  • J. Wenham, "The Identification of Luke", Evangelical Quarterly 63 (1991), 3–44

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwinjili Luka kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.