Kanisa kuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upande wa mbele wa Basilika kuu la Mt. Yohane huko Laterano wakati wa usiku. Ndilo kanisa kuu la Roma. Juu ya paa, pamoja na nyingine, kuna sanamu ya Yesu Mkombozi tena 12 za Mitume wa Yesu.
Kanisa kuu la Kilutheri la Helsinki, Ufini.
Kanisa kuu la Kikatoliki huko Salta, Argentina.

Kanisa kuu ni jina la heshima la jengo la ibada la madhehebu mbalimbali ya Ukristo ambalo Askofu wa jimbo (dayosisi) fulani analitumia kwa kawaida kutekeleza kazi yake kama mchungaji mkuu wa waamini wake, kama vile kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu, kutakasa watu kwa sakramenti na sala mbalimbali na kuwaunganisha wote katika kumfuata Yesu pamoja.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina hilo linashuhudiwa tayari na maandishi ya mwaka 516.

Linaitwa pia "kanisa mama" kwa sababu ni kama mama wa makanisa yote ya jimbo hilo.

Upekee[hariri | hariri chanzo]

Ndani yake umo ukulu, yaani kiti cha Askofu kisichopatikana katika makanisa mengine.

Kanisa kuu la Wakatoliki wote[hariri | hariri chanzo]

Kwa kuwa imani ya Kanisa Katoliki ni kwamba Papa wa Roma ni mkuu wa maaskofu wote duniani, kanisa kuu la jimbo lake ni pia kanisa kuu la Wakatoliki wote. Ndiyo sababu mlangoni mwa basilika kuu la Laterano imeandikwa kwamba ndilo "kichwa na mama wa makanisa yote ya jiji na ya dunia nzima".

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa kuu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.