Kitabu cha Baruk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kitabu cha Baruku ni kimojawapo kati ya vitabu vyadeuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kadiri ya utangulizi wake (Bar 1:1-14), kiliandikwa na Baruku, karani wa nabii Yeremia, wakati wa uhamisho wa Wayahudi huko Babuloni katika karne ya 6 K.K..

Hata hivyo wataalamu wanaona kiliandikwa katika karne ya 2 K.K. moja kwa moja katika lugha ya Kigiriki, isipokuwa labda sehemu ya pili inatokana na andiko asili la Kiebrania.

Kitabu kinatuingiza katika Uyahudi wa mtawanyiko na kutuonyesha jinsi maisha ya kidini yalivyodumishwa kwa kuhusiana na Yerusalemu, kwa sala na kushika Torati.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Viungo vya nje [hariri]

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.