Wimbo Ulio Bora
Wimbo Ulio Bora (kwa Kiebrania שיר השירים Shir ha-Shirim), ni kitabu kimojawapo cha Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
[hariri] Utunzi wake
Ingawa mapokeo yanamtaja mfalme Solomoni kama mtunzi, wataalama wanaona ni kazi ya mwandishi wa karne ya 4 K.K. aliyekusanya nyimbo mbalimbali za mapenzi.
[hariri] Aina ya uandishi
Ni kati ya vitabu vya kishairi na vya pekee zaidi katika Biblia, kwa kuwa kinaimba mahaba ya wapenzi wawili, ambao wanatafsiriwa kama wawakilishi wa Mungu na taifa lake, kadiri ya moja kati ya mafundisho makuu ya ufunuo, linalotokana na nabii Hosea.
Ndio ujumbe wa kitabu: upendo kati ya mume na mke unaweza na kutakiwa kufanana na ule kati ya Yesu Kristo na Kanisa lake.
[hariri] Viungo vya nje
Kitabu cha Wimbo Ulio Bora katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)
Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.