Kitabu cha Mika
Kitabu cha Mika ni kimoja kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh.
Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Yaliyomo |
[hariri] Mwandishi na muda
Jina la nabii huyo, aliyefanya kazi wakati uleule wa nabii Isaya, mwishoni mwa karne ya 8 K.K., lina maana ya "Nani kama Mungu?".
[hariri] Muhtasari
Kitabu kinaweza kuwaganyika sehemu nne ambamo vitisho na ahadi vinapokezana:
- hukumu dhidi ya Israeli (Mik 1:2-3,12)
- ahadi kwa Siyoni (Mik 4:1-5,14)
- hukumu ya pili dhidi ya Israeli (Mik 6:1-7,7)
- matumaini (Mik 7:8-20)
[hariri] Dondoo maarufu
Tunavyosoma katika Injili ya Mathayo (2:1-6), dondoo la Mik 5:2 lilitumiwa na Wayahudi kutarajia ujio wa Masiya wa ukoo wa Mfalme Daudi kutoka Bethlehemu.
Dondoo lenyewe lilibainisha miaka 700 kabla ya Yesu kuzaliwa kwamba Bethlehemu hiyo ni ile ya Efrata, si nyingine yenye jina hilohilo: "Bali wewe, Betlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele".
[hariri] Viungo vya Nje
Kitabu cha Mika katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)
Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.