Kitabu cha Ruthu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Katika fujo ya miaka ya Waamuzi (Kitabu cha Waamuzi), habari ya kitabu hiki kifupi inatujenga: inahusu Ruthu, mwanamke Mpagani aliyeolewa na Mwisraeli huko ng’ambo ya mto Yordani.

Baada ya kufiwa mume wake akafuatana na mama mkwe hadi Betlehemu ili aolewe na ndugu wa marehemu na kumzalia mtoto kadiri ya sheria.

Huyo mtoto akawa babu wa mfalme Daudi.

Hivyo kwa uaminifu wake mwanamke huyo pia akatajwa katika Injili kama bibi wa Yesu (Math 1:5-6).

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

[hariri] Mazingira

Habari kuu ya kitabu cha Ruthu ilitokea wakati wa Waamuzi, lakini inafurahisha mojo, ikilinganishwa na hali mbaya ya kidini na kimaadili iliyoandikwa katika kitabu cha Waamuzi. Habari yenyewe inaonyesha kwamba imani kamili kwa Mungu na uangalifu na upendo kwa watu wengine wakati ule pia ulikuwepo katika Israeli. Katika taifa zima walikuwepo watu wengine waliojitahidi kuishi maisha ya unyenyekevu na haki mbele ya Mungu wa kweli. Habari hiyo pia inaonyesha kwamba Mungu aliwaangalia watu kama hao kwa neema yake kubwa, akiyaongoza mambo yao ya kila siku na kuwafanikisha. Wema huo pia ulikuwa baraka kwa taifa zima.

[hariri] Yaliyomo

1:1-22 Miaka kumi ya taabu katika nchi ya Moabu 2:1-4:22 Mwanzo wa maisha mapya katika Israeli

[hariri] Viungo vya nje

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine