Kitabu cha Yona
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kitabu cha Yona ni kimojawapo kati ya vitabu vinavyounda Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), kwa hiyo pia Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo
Yaliyomo |
[hariri] Mahali pake katika Biblia
Tokea zamani kitabu hicho kimepangwa kati ya "Manabii wadogo" kwa sababu mhusika mkuu amepewa jina la nabii mmojawapo wa zamani.
Hata hivyo hakileti ujumbe wa kinabii, bali kinafanana zaidi na hadithi zenye fundisho la imani au maadili, kama vingine vilivyopangwa kati ya "vitabu vya historia".
Habari ni kwamba mtu huyo, alipopata wito wa kinabii kwa faida ya Waashuru wa mji wa Ninawi, maadui wa Israeli, alijaribu kuukwepa.
Baadaye, alipolazimika kuwatangazia adhabu ya Mungu, alionyesha huzuni kali kwa kuona wametubu na kuhurumiwa na Mungu.
[hariri] Lengo la kitabu
Lengo kuu la kitabu ni kupambana na utaifa wa Wayahudi uliowafanya wadhani Mungu anatakiwa kuwapenda wao tu, hata kusikitikia huruma yake kwa watu wa mataifa.
[hariri] Mwangwi katika Agano Jipya
Yona anatajwa katika Injili kuhusiana na ishara yake iliyomuashiria Yesu.
Kwanza, kwa kuhubiri pasipo miujiza, alionyesha mtu anapaswa kupokea ujumbe wa Mungu bila ya kumdai ishara inayothibitisha ukweli wake.
Pili, kwa kuwemo siku tatu tumboni mwa nyangumi, alifanywa ishara ya Yesu Kristo aliyekaa hadi siku ya tatu ndani ya kaburi.
[hariri] Ufafanuzi wake
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
[hariri] Viungo vya Nje
Kitabu cha Yona katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)
Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.