Martin Luther

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Martin Luther mwenye umri wa miaka 46

Martin Luther (10 Novemba 148318 Februari 1546) alikuwa Mkristo mwanateolojia kutoka nchi ya Ujerumani.

Alijiunga na shirika la watawa wa mtakatifu Augustino, akawekwa wakfu kama kasisi na kuwa profesa wa Biblia kwenye chuo kikuu cha Wittenberg.

Universität Wittenberg

Swali lililomtesa kwa muda mrefu, yaani "Vipi nimpate Mungu mwenye huruma?", lilijibiwa aliposoma Waraka kwa Waroma, sura ya 3, mstari wa 24: "kwa zawadi ya neema ya Mungu, watu wote hukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Yesu Kristo anayewakomboa."

Hapo alianza kupinga mafundisho ya Kanisa kuhusu stahili za matendo mema.

Tarehe 31 Oktoba 1517, alitolea kimaandishi "Hoja 95 dhidi ya rehema" (kwa Kijerumani: 95 Thesen wider den Ablass).

Hii ilimfanya ashindane hata na Papa wa Roma, na kutengwa na Kanisa Katoliki akiongoza Matengenezo ya Kiprotestanti yaliyosababisha mapema madhehebu mengi mapya kutokana na wazo kuu la kwamba Biblia inajitegemea na kumtosha kila anayesoma.

Aliandika vitabu vingi, kutunga nyimbo kadhaa na hasa kutoa tafsiri Biblia ya Kikristo katika lugha ya Kijerumani.

Athari yake imekuwa kubwa sana katika Kanisa na ulimwengu kwa jumla.

Viungo vya nje [hariri]

People.svg Makala hii kuhusu mtu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Martin Luther kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.