Waaugustino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Waaugustino ni hasa watawa wanaofuata kanuni ya Agostino wa Hippo. Kwa Kilatini shirika lao linaitwa Ordo Fratrum Sancti Augustini. Tangu muda mrefu linahesabiwa kati ya mashirika ya ombaomba.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Katika karne XII zilikuwepo jumuia nyingi zilizofuata kanuni hiyo. Katikati ya karne XIII, kwa juhudi za kardinali Riccardo Annibaldi, ulianza mchakato wa kuziunganisha.

Tarehe 16 Desemba 1243 Papa Inosenti IV alitoa hati Incumbit nobis ili kuhimiza mchakato huo, hata Machi 1244 shirika likaanzishwa.

Baadhi ya Waaugustino katika karne zilizofuata walifanya juhudi za urekebisho na kuanzisha matawi mapya.

Takwimu[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 31 Desemba 2005, mbali na matawi hayo yaliyojitegemea, shirika lilikuwepo katika mabara yote likiwa na konventi 448 na watawa 2.803, ambao 2.088 kati yao walikuwa mapadri.[1]

Kati ya nchi 24 ambako shirika linaishi, kuna Kenya na Tanzania.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Takwimu kutoka'Annuario Pontificio per l'anno 2007, Città del Vaticano, 2007, uk. 1466.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]