Kardinali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
StPetersBasilicaEarlyMorning.jpg
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria
Kukingiwa dhambi ya asili Kupalizwa
Dhambi Purgatorio


Muundo

Papa: Benedikto XVI
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa liturujia
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Milano Lyon Toledo)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Kigiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Mavazi ya kardinali yaonyesha rangi nyekundu (hapa kwenye dirisha la duka la mavazi ya kikanisa huko Roma)

Kardinali ni cheo cha juu katika Kanisa Katoliki.

Yaliyomo

[hariri] Wenye kumchagua Papa

Mkutano wa makardinali humchagua Papa mpya ambaye ni mkuu wa kanisa hili ambayo ni madhehebu ya Kikristo kubwa kuliko jumla ya mengine yote duniani. Uchaguzi hutokea baada ya papa aliyetangulia kufa au kujiuzulu. Kati ya kifo cha papa na uchaguzi wa mwandamizi wake ni mkutano wa makardinali unaoongoza kanisa lote kwa muda. Lakini kardinali aliyefikia umri wa miaka 80 hashiriki tena katika uchaguzi wa Papa.

[hariri] Uteuzi wa kardinali

Kwa kawaida kardinali huteuliwa kati ya maaskofu lakini kuna pia makasisi wachache wanaoteuliwa na papa kuwa kardinali bila ya kupewa uaskofu.

Mwenye kuteua kardinali ni papa peke yake, naye ana haki ya kumteua kardinali bila ya kutangaza jina lake. Kardinali ya aina hii huitwa kwa Kilatini "in pectore" (moyoni). Hii inaweza kutokea hasa kama ni kardinali kutoka nchi pasipo na uhuru wa kidini au nchi ambayo haina uhusiano mzuri na kanisa katoliki.

[hariri] Wajibu wa kardinali

Wajibu kubwa ni wakati wa kifo cha Papa kumchagua mwandamizi wake.

Kuna idadi ya makardinali wanaoishi Vatikani. Kwa kawaida viongozi wa idara za Vatikani wapewa kofia ya kardinali.

[hariri] Idadi ya makardinali

Hakuna idadi maalumu ya makardinali na mnamo 24 Novemba 2007 wako 201. Lakini Papa Paulo VI aliunda utaratibu kuwa wasiwepo zaidi ya makardinali 120 wenye haki ya kupiga kura. Wale waliofikia umri wa miaka 80 hawashiriki tena katika uchaguzi wa papa mpya. Lakini kardinali hajiuzulu wala kustaafu: anaendelea na cheo na pia na haki ya kushiriki katika mkutano wa makardinali hadi kifo.

Kimapokeo makardinali wengi ni Waitalia, hata mapapa walikuwa Waitalia watupu kwa karne nne hadi Papa Yohane Paulo II. Lakini asilimia ya makardinali Waitalia imepungua; kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia zaidi ya nusu walikuwa Waitalia, siku hizi ni takriban asilimia 20. Kwa sasa makardinali wanatokea nchi 70 za mabara yote. Kati yao wenye haki ya kupiga kura wanatokea nchi 52.

Mgawanyo wa makardinali kwenye mabara ni kama ufuatao:

[hariri] Tazama pia


WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Kardinali" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Kardinali kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.