Urika wa maaskofu
Urika wa maaskofu ni msamiati wa teolojia ambao unatokeza imani ya Kanisa katika umoja wa sakramenti ya Daraja takatifu katika ngazi yake ya juu kuhusu utekelezaji wa kazi tatu ambazo Yesu aliwaachia Mitume wake na waandamizi wao kwa njia yao.
Maaskofu wote wanaunda kundi hilo kutokana na sakramenti waliyopokea, hata wasipoongoza jimbo lolote.
Katika utekelezaji wake, Kanisa Katoliki linadai daima uwepo wa mkuu wa kundi la maaskofu, yaani askofu wa Roma akiwa mwandamizi wa mtume Petro ("cum et sub Petro").
Fundisho hilo, lililosisitizwa na Mtaguso wa pili wa Vatikano, linatekelezwa hasa katika Mtaguso mkuu, lakini pia katika Sinodi ya maaskofu]] na miundo mingine ya ushirikiano.
Yanayohusu urika wa maaskofu katika Mkusanyo wa Sheria za Kanisa la Kilatini wa mwaka 1983 yanapatikana katika kitabu II, sehemu II, kanuni 336-341.