Urekebisho wa Kikatoliki
Urekebisho wa Kikatoliki ulikuwa kipaumbele cha Wakristo wengi wa Kanisa Katoliki hasa katika karne XV na XVI.
Juhudi hizo zilikuwa na upana mkubwa na kuhusu kwa namna ya pekee mambo matano yafuatayo:
- Mafundisho ya imani
- Miundo ya Kanisa
- Utawa
- Matapo ya kiroho
- Majukumu ya kisiasa
Juhudi hizo zilipata nguvu mpya baada ya Matengenezo ya Kiprotestanti (yaliyoanzishwa na Martin Luther) kupamba Ulaya Kaskazini kuanzia Ujerumani. Kwa sababu hiyo ukaja kuitwa (1776) 'Counter-Reformation'.
Juhudi hizo zilipitishwa na Mtaguso wa Trento, ambao ndio mtaguso mkuu wa Kanisa Katoliki uliodumu muda mrefu zaidi (1545–1563) na kutoa mafundisho na maagizo mengi zaidi. Katika hayo upande mmoja ilionekana nia ya kupokea baadhi ya hoja za Waprotestanti, ambao kwa wakati huo walikuwa wameshaganyika makundimakundi, upande mwingine ilionekana nia ya kutetea imani sahihi ya mapokeo ya mitume pale ambapo msimamo wao ulitazamwa kuwa uzushi, kwa mfano kuhusu sakramenti.