Liturujia ya Braga
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Liturujia ya Braga ni liturujia maalumu ya jimbo la Braga (Ureno) inayotumika tangu karne ya 6.
Inahusiana na aina nyingine za liturujia ya Kilatini, kama vile liturujia ya Toledo na liturujia ya Roma.
Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano, jimbo la Braga limeamua (1971) kuendelea na liturujia hiyo pamoja na ile ya Roma.