Amri Kumi
Kutoka Wikipedia
Amri Kumi ni orodha za amri za kidini katika Biblia kitabu cha Kutoka 20:1-17.
Amri hizi ni sehemu ya Torati ya Kiyahudi na kukubaliwa pia na Wakristo walio wengi kama amri zinazohusu pia Wakristo.
[hariri] Maneno ya Amri Kumi
Maneno ya Kutoka 20:1-17 kufuatana na tafsiri ya Biblia ya Union Version ni kama yafuatayo (namba za mbele ni hesabu ya amri kumi, namba zinazofuata ni hesabu ya aya za sura 20):
(20:1) Mungu akanena maneno haya yote akasema:
(20:2) Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
- (20:3) Usiwe na miungu mingine ila mimi.
- (20:4) Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. (20:5) Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi. BWANA Mungu wako, ni Mungu wenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, (20:6) nami nawerehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
- (20:7) Usilitaje bure jina la BWANA hatamhesabiwa kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
- (20:8) Ikumbuke siku ya sabato uitakase. (20:9) Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; (20:10) lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya mlango yako. (20:11) Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
- (20:12) Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
- (20:13) Usiue.
- (20:14) Usizini.
- (20:15) Usiibe.
- (20:16) Usishuhudie jirani yako uongo.
- (20:17) Usiitamani nyumba ya jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

