Makanisa Katoliki ya Mashariki
Makanisa Katoliki ya Mashariki ni madhehebu 23 ya Ukristo ambayo yanafuata mapokeo mbalimbali ya Mashariki katika ushirika kamili na Askofu wa Roma (Papa), hivyo pia na Kanisa Katoliki lote duniani.
Mapokeo hayo ni hasa yale ya Aleksandria (Misri), Antiokia (kihistoria jiji la Siria, leo nchini Uturuki), Konstantinopoli (kihistoria jiji la Ugiriki, leo nchini Uturuki), Armenia na Wakaldayo (kihistoria Mesopotamia, leo Iraq).
Baadhi ya mapokeo hayo yamezaa matawi, kama lile la Ethiopia.
Pamoja na hayo, kama Makanisa ya Waorthodoksi, hayo yanaambatana na utamaduni wa taifa, na kuyafanya yagawanyike kiutawala hata kama teolojia, liturujia n.k. zinaendelea kuwa zilezile kadiri ya mapokeo. Kwa jumla yanakubali mapadre waliooa lakini hawana maaskofu waliooa.
Yaliyomo |
Historia [hariri]
| Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu Kanisa Katoliki |
|
| Imani | |
|---|---|
|
Umoja wa Mungu |
|
| Muundo | |
|
Papa: Benedikto XVI |
|
| Historia | |
|
Historia Ukristo |
|
| Ibada | |
| Mapokeo ya liturujia | |
|
Liturujia ya Kilatini (Roma Milano Toledo Braga Lyon Canterbury) |
|
Chanzo cha Wakatoliki wa Mashariki ni tofauti: baadhi (hasa wale wa Kanisa la Wamaroni) wanadai kuwa wamedumu tangu mwanzo katika ushirika kamili na Papa, au walijikuta hawana tena mawasiliano na Patriarki wao kutokana na hali ya siasa, hivyo wakaanza kushirikiana na Kanisa la Kilatini (hasa Kanisa la Waalbania wa Italia). Wengine wametokana na makubaliano kati ya Papa na baadhi ya Waorthodoksi walioona umuhimu wa kuwa na umoja naye, hata wakakubali kutengana na Makanisa yao ya asili (kwa mfano Kanisa la Kisirya la Malankara).
Kwa mengine mengi ni kwamba siku za nyuma kulikuwa na majaribio mbalimbali ya Mapapa ya kuunganisha Makanisa ya Kiorthodoksi na Kanisa la Roma baada ya mafarakano yaliyotokea hasa katika karne ya 5. Majaribio hayo kwa jumla yalishindikana, lakini pengine yalisababisha mafarakano mapya katika makanisa ya Kiorthodoksi ambamo askofu fulani alikubali mamlaka ya Papa na kuungana na Kanisa la Roma pamoja na wafuasi wake. Mara kadhaa hao walikuwa wanagombea vyeo vikuu katika Makanisa ya Kiorthodoksi, halafu wakaamua kuungana na Papa baada ya kutochaguliwa katika makanisa yao ya asili. Kwa sababu hiyo, wanatazamwa vibaya na Waorthodoksi.
Siku hizi Kanisa Katoliki limetamka wazi kwamba halina tenga mipango kama hiyo katika kulenga umoja na madhehebu mengine, bali linafuata njia za ekumeni.
Mtaguso wa pili wa Vatikano uliyazungumzia Makanisa Katoliki ya Mashariki na kuyatolea hati "Orientalium Ecclesiarum" ili yastawi upya na kuwa daraja kati ya Wakatoliki na Waothodoksi.
Takwimu [hariri]
Kuna Makanisa 23 yaliyoungana hivyo na Roma. Kati ya hayo makubwa zaidi ni:
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina
- Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar
- Kanisa la Wamaroni
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Wamelkiti
Katika Afrika yako hasa Makanisa ya:
- Kanisa Katoliki la Kiethiopia (nchini Ethiopia na Eritrea)
- Kanisa Katoliki la Kikopti (nchini Misri)
Leo Wakatoliki wa Mashariki ni asilimia 2 ya Wakatoliki wote, yaani kwa jumla kuna takriban Wakristo milioni 20 katika makanisa haya.
Kati yao wengi wanafuata mapokeo ya Kisiria na ya Kigiriki.
Uongozi [hariri]
Kwa kawaida Makanisa hayo yangetakiwa kuongozwa na Patriarki, lakini upinzani wa Waorthodoksi umefanya Papa asiyapatie cheo hicho yale yasiyokuwa nacho tayari. Badala yake kilibuniwa kile cha Askofu mkuu kabisa, ambacho kina mamlaka karibu sawa katika madhehebu makubwa 4: Waukraina, Wasiro-Malabari, Wasiro-Malankara na Waromania.
Mengi ya makanisa haya yanakubali kuwapa upadri waamini waliooa, lakini maaskofu na sehemu ya mapadri hawaoi. Kwa kawaida wanachagua maaskofu wao wenyewe watakaothibitishwa na Papa, tofauti na Wakatoliki wengi katika Kanisa la Kilatini ambako ni Papa anayemteua askofu mpya moja kwa moja.
Orodha [hariri]
- Makanisa sui iuris yanayofuata mapokeo ya Kigiriki ni 15):
- Kanisa Katoliki la Waalbania wa Italia (Italia)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Albania (Albania)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Belarus (Belarus)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Bulgaria (Bulgaria)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Korasya (Croatia)
- Kanisa Katoliki la Kibizanti la Ugiriki (Ugiriki na Uturuki)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Serbia na Montenegro (Serbia na Montenegro)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Masedonia (Macedonia)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kimelkiti (Siria, Lebanon, Israel, Palestina, Jordan, Iraq, Kuwait, Misri, Sudan, Marekani, Kanada, Mexiko, Venezuela, Brazil, Argentina n.k.)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania (Romania, Marekani)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kiruteni (Ukraina, Marekani, Ucheki)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Russia (Russia na China)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Slovakia (Slovakia, Kanada)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina (Ukraina, Poland, Marekani, Kanada, Brazil, Argentina, Ufalme wa Muungano, Ujerumani na Skandinavia, Ufaransa, Australia, n.k.)
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Hungaria (Hungaria)
- Makanisa sui iuris yanayofuata mapokeo ya Aleksandria (2)
- Kanisa Katoliki la Wakopti (Misri)
- Kanisa Katoliki la Waethiopia (Ethiopia na Eritrea)
- Makanisa sui iuris yanayofuata mapokeo ya Antiokia (3)
- Kanisa la Wamaroni (Lebanon, Siria, Kupro, Israel, Palestina, Misri, Jordan, Argentina, Brazil, Marekani, Kanada, Mexiko, Australia n.k.)
- Kanisa Katoliki la Kisiria (Lebanon, Iraq, Jordan, Kuwait, Palestina, Misri, Sudan, Syria, Uturuki, Marekani, Kanada, Venezuela n.k.)
- Kanisa Katoliki la Kisiria la Malankara (India)
- Makanisa sui iuris yanayofuata mapokeo ya Mesopotamia (2)
- Kanisa Katoliki la Wakaldayo (Iraq, Iran, Lebanon, Jordan, Palestina, Misri, Siria, Uturuki, Marekani)
- Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar (India, Marekani)
- Kanisa sui iuris linalofuata mapokeo ya Armenia (1)
- Kanisa Katoliki la Armenia (Armenia, Georgia na nchi nyingine zilizokuwa zinaunda Urusi, Lebanon, Iran, Iraq, Misri, Syria, Uturuki, Israel, Palestina, Ugiriki, Romania, Ukraina, Ufaransa, Argentina na nchi nyingine za Amerika ya Kilatini, Marekani, Kanada n.k.)
Viungo vya nje [hariri]
Kwa jumla [hariri]
- Hati Orientalium Ecclesiarum ya Mtaguso wa pili wa Vatikano
- Hati Orientales omnes Ecclesias ya Papa Pius XII
- Orientale Lumen - Hati ya Papa Yohane Paulo II kuhusu Makanisa ya Mashariki
- Codex Canonum Ecclesiarum Orientalium - Mkusanyo wa Sheria za Makanisa ya Mashariki (katika Kilatini pamoja na sehemu sambamba)
- Instruction for Applying the Liturgical Prescriptions of the Code of Canons of the Eastern Churches - Hati ya Idara ya Papa kwa Makanisa ya Mashariki kuhusu liturujia
- Ujuzi wa msingi kuhusu Makanisa hayo
- Makanisa Katoliki ya Mashariki huko Marekani
- CNEWA Idara ya Papa inayosaidia Makanisa hayo
- Sura ya Idara ya Papa kwa Makanisa hayo
- Takwimu za Makanisa hayo,
+
Moja moja [hariri]
- Kanisa la Wamaroni Tovuti rasmi
- Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar Tovuti rasmi
- Kanisa Katoliki la Kibizanti nchini Marekani Tovuti isiyo rasmi
- Kanisa Katoliki la Waarmenia Tovuti rasmi
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania Tovuti rasmi
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Hungaria Tovuti rasmi
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kimelkiti Tovuti rasmi
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina Tovuti rasmi
- Kanisa Katoliki la Kisiria la Malankara Tovuti rasmi
- Kanisa Katoliki la Kisiria la Malankara
- Jimbo kuu la Kibizanti la Pittsburgh Tovuti rasmi
- Kanisa la Kibizanti la Ugiriki
- Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania