Pennsylvania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ramani ya Pennsylvania
Ramani ya Pennsylvania
Mahali pa Pennsylvania katika Marekani
Mahali pa Pennsylvania katika Marekani

Pennsylvania ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika kaskazini-mashariki ya nchi ikipakana na majimbo ya Ohio, West Virginia, Maryland, Delaware, New Jersey na jimbo la New York. Kona ya kaskazini-magharibi yagusa Ziwa Erie na Kanada iko ng'ambo ya ziwa hili.

Mji mkuu ni Harrisburg lakini mji mkubwa ni Philadelphia.

Jina la jimbo latokana na William Penn aliyepewa hapa ardhi ya kuanzisha makazi kwa ajili ya kundi la kidini cha Maquaker. Jina la jimbo latafsiriwa kama "misitu ya Penn". Ilikuwa moja ya koloni 13 asilia za Uingereza zilizoasi dhidi ya nchi mama baada ya mwaka 1776 na kuanzisha Maungano ya Madola ya Amerika .

Pennsylvania ina wakazi 12,281,054 kwenye eneo la 119,283 km². Zaidi ya nusu huishi katika maeneo ya miji mikubwa Pittsburgh na Philadelphia. Kaskazini ya jimbo ina watu wachache.

Sehemu kubwa ya eneo la jimbo ni milima ya Appalachi. Mito mikubwa ni Monongahela, Allegheny na Ohio.



Majimbo na maeneo ya Marekani
Majimbo ya Marekani
AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming
Mkoa wa Mji Mkuu
Mkoa wa Columbia (Washington D.C.)
Visiwa vya ng'ambo
Katika Pasifiki: Samoa ya MarekaniVisiwa vya Mariana ya KaskaziniGuamKatika Karibi: Puerto RicoVisiwa vya Virgin vya MarekaniVisiwa vidogo sana vya Pasifiki:Kisiwa cha HowlandKisiwa cha JarvisAtolli ya JohnstonKingman ReefAtolli ya MidwayKisiwa cha BakerAtolli ya PalmyraKisiwa cha WakeKisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa
Vifaa binafsi