Maryland
| Maryland | |||
| Mahali pa Maryland katika Marekani | |||
|
|||
| Nchi | |||
|---|---|---|---|
| Mji mkuu | Annapolis | ||
| Eneo | |||
| - Jimbo | 32,133 km² | ||
| - Bara | 25,314 km² | ||
| - Maji | 6,819 km² | ||
| Tovuti: http://www.maryland.gov/ | |||
Maryland ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko kwenye pwani la Atlantiki upande wa mashariki ya Marekani bara. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, West Virginia, Delaware, Virginia na mkoa wa shirikisho la Washington DC.
Hori la Chesapeake linagawa eneo la jimbo kwa pande mbili. Mji mkuu ni Annapolis na mji mkubwa ni Baltimore. Kwa miji mingine, angalia orodha ya miji.
Iliundwa kama koloni ya Ungereza mwaka 1634 na mkabaila Lord Baltimore aliyetumia jina la Maryland kwa heshima ya mke wa mfalme Charles I. Baltimore aliyetoka Ueire alitafuta hasa mahali kwa ajili ya Wakatoliki wasiokubaliwa katika koloni nyingine za Uingereza. Maryland ilikuwa koloni ya kwanza yenye sheria iliyokubali madhehebu yote ya kikristo.
Mji mkuu wa Washington DC ulijengwa kwenye eneo lililotengwa na eneo la Mayrland kando la mto Potomac. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani 1861-1865 Maryland ilikaa upande wa Maungano.
Viungo vya Nje [hariri]
- State of Maryland (tovuti ya serikali)
- USGS habari za Maryland
- U.S. idara ya sensa
| Majimbo ya Marekani |
|---|
|
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Maryland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |