Hori ya Chesapeake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Hori ya Chesapeake

Hori ya Chesapeake (kwa Kiingereza: Chesapeake Bay) ni hori ya Atlantiki nchini Marekani na pia mdomo wa pamoja wa mito kadhaa hasa mto Susquehanna. Imepakana na majimbo ya Virginia na Maryland.

Eneo lake ni km² 12,000 na inapokea maji ya mabeseni ya mito inayoishia humo zenye jumla ya km² 165,800. Kijiolojia hori ni mwendo wa kale wa mto Susquehanna uliochimbwa miaka 15,000 iliyopita wakati wa enzi ya barafu ambako uwiano wa bahari ulikuwa mita 100 chini ya uwiano wa leo. Baada ya kupanda kwa uso wa bahari maji yake yalijaa katika bonde la mto na kulifanya kuwa hori ya Atlantiki.

Sehemu nyembamba ya hori iko karibu na mji wa Annapolis, Maryland penye daraja la Bay Bridge. Karibu na mdomo kuna handaki chini ya ardhi na chini ya bahari inayounganisha barabara pande zote mbili.

Bay Bridge

Mito inayoishia horini[hariri | hariri chanzo]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Hori ilikuwa mahali pa mapigano kati ya manowari za Ufaransa na Uingereza mwaka 1781. Wafaransa walizuia jeshi la Uingereza lisiongeze wanajeshi kutoka manowari zake likasaidia Wamarekani kushinda vita ya uhuru wa Marekani.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons