Liturujia ya Vipindi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Liturujia ya Vipindi ni sala rasmi ya Kanisa kama inavyoadhimishwa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo.

Kwa njia yake waamini wa Yesu wanaungana naye katika sala yake ya kudumu.

Inaitwa hivyo kwa sababu inafanyika kwa vipindi mbalimbali kadiri ya mwendo wa siku (usiku na mchana): muhimu zaidi ni vipindi vya asubuhi na jioni.

Katika Kanisa la Kilatini hiyo sala ya Kanisa inategemea hasa Biblia ya Kikristo kwa kutumia Zaburi na masomo kutoka kwake.