Maisha ya kiroho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maisha ya Kiroho ndiyo maisha maisha ya kuongozwa na Roho Mtakatifu nyuma ya Yesu Kristo kwa utukufu wa Mungu Baba.

Ufuasi huo unafanyika pamoja na wengine katika Kanisa, jumuia ya wanafunzi wa Yesu inayotokana na kundi la kwanza la Mitume wake.

Mwanzo wake wa kawaida ni ubatizo, uliofananishwa na Yesu mwenyewe na aina ya kuzaliwa upya kwa maji na Roho Mtakatifu.

Maisha hayo yanalishwa mfululizo na Neno la Mungu na ekaristi.

Lengo ni kufikia muungano na Mungu katika uzima wa milele, lakini huo unaanzia hapa duniani katika ustawi wa maadili makuu ya imani, tumaini na upendo, pamoja na vipaji vya Roho Mtakatifu

Teolojia hiyo ya maisha ya kiroho ya Kikristo inaitwa pia kifupi Teolojia ya Kiroho.

Nje ya Ukristo, dini mbalimbali zinazungumzia maisha ya kiroho kama namna ya kuishi kadiri ya roho, si kadiri ya mwili tu.

[hariri] Viungo vya nje