Kiboko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiboko
Kundi la viboko mtoni Luangwa (Zambia)
Kundi la viboko mtoni Luangwa (Zambia)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Nusungeli: Placentalia (Wanyama wenye mji)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye kwato mbili kwa kila mguu)
Nusuoda: Suina
Familia: Hippopotamidae (Wanyama walio na mnasaba na kiboko)
Jenasi: Hippopotamus Linnaeus, 1758
Spishi: H. amphibius Linnaeus, 1758

Kiboko (Hippopotamus amphibius) ni mamalia mkubwa wa familia ya Hippopotamidae. Nyumbani kwake ni bara la Afrika. Huishi kwenye maji ya mito na maziwa lakini ina uwezo wa kutembea kwenye nchi kavu mbali na maji. Chakula chake ni majani.

Kimo cha mbegani kinafikia mita 1.5 na urefu wake hadi mita 4.5. Uzito wake ni kati ya kilogramu 2700 na 4500 kg. Hivyo kiboko inashindana na kifaru juu ya cheo cha kuwa mnyama mzito wa pili kwenye nchi kavu baada ya tembo. Akikimbia hufikia mwendo wa lilomita 48 kwa saa ingawa kwa muda mdogo tu.