Karne ya 14

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Karne ya 14 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1301 hadi 1400. Kikamilifu kilianza tar. 1 Januari 1301 na kuishia 31 Desemba 1400. Namba zake zinafuata hesabu ya miaka "baada ya Kristo".

Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya kibinadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu - hali halisi maendeleo na mabadiiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.

Kuna mambo mengi yaliyotokea wakati wa karne hii.

Watu na matukio[hariri | hariri chanzo]

Karne: Karne ya 13 | Karne ya 14 | Karne ya 15
Miongo na miaka
Miaka ya 1300 | 1300 1301 1302 1303 1304 1305 1306 1307 1308 1309
Miaka ya 1310 | 1310 1311 1312 1313 1314 1315 1316 1317 1318 1319
Miaka ya 1320 | 1320 1321 1322 1323 1324 1325 1326 1327 1328 1329
Miaka ya 1330 | 1330 1331 1332 1333 1334 1335 1336 1337 1338 1339
Miaka ya 1340 | 1340 1341 1342 1343 1344 1345 1346 1347 1348 1349
Miaka ya 1350 | 1350 1351 1352 1353 1354 1355 1356 1357 1358 1359
Miaka ya 1360 | 1360 1361 1362 1363 1364 1365 1366 1367 1368 1369
Miaka ya 1370 | 1370 1371 1372 1373 1374 1375 1376 1377 1378 1379
Miaka ya 1380 | 1380 1381 1382 1383 1384 1385 1386 1387 1388 1389
Miaka ya 1390 | 1390 1391 1392 1393 1394 1395 1396 1397 1398 1399

Karne ya saa za kwanza[hariri | hariri chanzo]

Labda badiliko kubwa lilikuwa uenezi wa saa za kimekanika kwenye minara ya miji ya Ulaya. Tofauti na saa za jua au saa za maji ziliwaonyesha watu wengi wakati tena bila ya kutegemea hali ya hewa. Wataalamu wengi huamini ya kwamba hakuna mitambo mingine iliyobadilisha utamaduni wa binadamu kuliko saa.

Karne ya kifo katika Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Ulaya iliathiriwa mara ya kwanza na ugonjwa wa kuambukiza wa tauni. Tauni iliua wakulima wengi ikasababisha njaa kali; zote pamoja zikaua zaidi ya theluthi ya wakazi wote wa Ulaya. Vifo vingi vilisababisha hofu kubwa kati ya watu. Wayahudi walishtakiwa kuwa sababu ya maradhi na vifo wakauawa na kudhulumiwa katika nchi nyingi za Ulaya.

Uenezaji wa milki ya Waturuki Waosmani[hariri | hariri chanzo]

Udhaifu wa Ulaya katika karne hii ilisaidia uenezaji wa milki ya Waturuki Waosmani kutoka Anatolia kujiandaa kuingia nchi za Balkani (Ulaya ya Kusini-Mashariki). Hivyo utawala wa Kiislamu ulielekea kuenea hata katika mashariki ya Ulaya utakaokuwepo kwa karne tano zilizofuata. Baadaye athira yake ilifikia pwani za Uswahilini na Uganda.

Milki za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Katika Afrika ya Magharibi Wahaussa wanaunda milki zao za kwanza. Mali inapanuka. Majengo makubwa ya Zimbabwe Kuu yanaanzishwa.