Ualimu wa kanisa
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ualimu)
Kwa jina hilo Kanisa Katoliki linamaanisha mamlaka yake ya kufundisha ili kudumisha, kustawisha na kueneza karne hadi karne hazina ya imani iliyofunuliwa na Mungu hasa katika Yesu Kristo na kukabidhiwa kwa Mitume wake.
Ualimu unaweza kuwa wa kawaida na usio wa kawaida.
Ule wa kawaida ndiyo namna ambayo Papa na Maaskofu wenzake wanatoa mafundisho yao siku kwa siku kwa njia ya hotuba, barua na maandishi mengine.
Kumbe ule usio wa kawaida unatolewa kwa fahari ya pekee, kwa mfano katika Mtaguso au katika tamko rasmi la kudumu linalotolewa na Papa kwa niaba ya Maaskofu wote.

