Sefania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Nabii Sefania (kwa Kiebrania צְפַנְיָה yaani "Aliyefichwa na Mungu"), alikuwa mwana wa Kushi, mtu wa Yerusalemu aliyehubiri kwa nguvu miaka 640-625 hivi K.K. yaani mwanzoni mwa utawala wa mfalme Yosia, kabla huyo hajaanza urekebisho wake wa kidini uliofuata kuvumbua hekaluni maandiko ya Kumbukumbu la Sheria.

Ni wakati uleule aliofanya kazi nabii Yeremia, ambaye analingana naye sana.

Habari zake zinatokana tu na kitabu chake Kitabu cha Sefania ambacho ni cha tisa kati ya vile 12 vya Manabii Wadogo.

Pamoja na kutisha kwa matabiri yake dhidi ya maovu ya watu wa Yuda, aliahidi wokovu kwa mabaki ya Israeli, akisema watakuwa watu maskini na walionewa (3:9-20).

Ndio mwanzo wa imani ya kuwa wapenzi wa Mungu ni hasa mafukara, atakavyosisitiza Yesu (Lk 6:20-21).

Saint-stub-icon.jpg Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sefania kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine