M
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Alfabeti ya Kilatini | ||||||
|---|---|---|---|---|---|---|
| Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
| Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
| Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
| Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
| Ww | Xx | Yy | Zz | |||
M ni herufi ya 13 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Mi ya alfabeti ya Kigiriki.
[hariri] Maana za M
- Kama kipimo sanifu cha kimataifa m humaanisha mita kama kiwango cha umbali.
- Kati ya namba za Kiroma M ni alama kwa 1,000
- kwenye gari M ni alama ya kimataifa ya gari kutoka Malta
- katika fizikia m ni alama ya masi (ling. E=mc2)
- katika falaki majina ya nyota na magimba mengine ya angani hutajwa kwa M pamaoja na namba ya Orodha ya Messier
- Katika filamu za James Bond M ni kifupi cha mkubwa wa upelelezi wa Uingereza
[hariri] Historia ya alama M
| Kisemiti asilia: picha ya maji |
Kifinisia: Mem kwa "M" |
Kigiriki Mi |
Kietruski M |
Kilatini M |
|---|---|---|---|---|
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Asili ya herufi M ni katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.
Wafinisia walikuwa na alama ya "Mem" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya maji wakitumia alama tu kwa sauti ya "m" na kuiita kwa neno lao kwa maji "mem". Kwa kurahisisha kazi ya kuandika waliongeza stari mrefu upande walipoanza kuandika.
Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "Mi" bila kujali maana asilia ya "maji" ilikuwa sauti tu ya "m". Waligeuza alama kulingana na mwendo wao wa kuandika kuanzia upande wa kushoto na kufikia umbo lililokaa hivyo.
Waitalia ya kwanza wakaipokea ilivyo hata kama walirudi mara nyingi kwa umbo la mapema.
Waroma wakaendeleza alama hiyo katika alfabeti yao kwa maana hiyihiyo.
| Makala hiyo kuhusu "M" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu M kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |



