L

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alfabeti ya Kilatini
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz


L ni herufi ya 12 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Lambda ya alfabeti ya Kigiriki.

[hariri] Maana za L

[hariri] Historia ya L

Kisemiti asilia
Fimbo la kuchungia ng'ombe
Kifinisia
Lamed
Kigiriki
Lambda
Kietruski
L
Kilatini
L
Proto-semiticL-01.png PhoenicianL-01.png Lambda uc lc.svg EtruscanL-01.png RomanL-01.png

Asili ya alama ni picha andishi iliyoonyesha fimbo la kuchungia ng'ombe. Wafinisia walirahisihsa alama hiyo na kuiita kwa neno lao la fimbo hili "lamed". Wakaitumia kama alama ya sauti "l". Wagiriki wa Kale wakaipokea kama "Lambda" na kubadilisha umbo lake kuwa kama paa ya nyumba.

Waetruski walipendelea umbo la kifinisia kwa kuiandika kama alama ya sauti "l". Waroma wa Kale wakageuza alama na kunyosha mikono yake kuwa L jinsi iliovyo hadi leo.

WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "L" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu L kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.