Y

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

Y ni herufi ya 25 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Ipsiloni ya alfabeti ya Kigiriki.

Maana za Y[hariri | hariri chanzo]


Historia ya Y[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Y ina asili za pamoja na U, W, V na F. Historia hii ni ngumu kidogo kwa sababu alama ilipita katika alfabeti za lugha ambazo zilitumia hasa alama hii kwa sauti tofautitofauti. Kwa sababu hii matamshi yalibadilika kati ya lugha na lugha. Pia lugha mpya iliweza kuona haja ya kuunda alama mpya kwa sauti ya pekee.

Kisemiti asilia
W
Kifinisia
Waw
Kigiriki
Ipsiloni
Kilatini
Y

Alama ya Y kiasili haikupatikana katika Kilatini cha Kale. Ilihitajika baada ya Roma kutawala Ugiriki na lugha ya Kilatini kupokea maneno mengi ya Kigiriki yaliyokuwa na herufi ya ipsiloni.

Asili yake ni "waw" ya Kifinisia iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya fimbo la kingoe au kiopoo. Wagiriki wa Kale walichukua alama hiyo na kuitumia kwa namna mbili: kwa umbo moja kama digamma (tazama F) na umbo la pili kama "ipsilon" bila kujali maana asilia ilitaja sauti kati ya "u" na "i".

Ipsiloni iliingia tayari mwanzoni katika alfabeti ya Kilatini kupitia Kietruski lakini kwa sauti ya "u/v". Kwa hiyo iliigizwa mara ya pili kwa maana yake ya Kigiriki.

Katika lugha kadhaa inaonyesha leo konsonanti (kama Kiswahili) katia lugha kadhaa huonyesha vokali kama "i" ya Kijerumani / Kituruki "ü". Katika Kiingereza ni mara konsonanti mara vokali.