Wafinisia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wafinsia walikuwa taifa la Nyakati za Kale walioishi kwenye mwambao wa mashariki wa Bahari ya Mediteranea. Miji-dola yao yalikaa katika eneo la nchi za kisasa Lebanoni na Syria.
Wafinisia walitumia Kifinisia kilichokuwa lugha ya Kisemiti ambayo ilipotea baada ya kusambaa kwa Kiarabu tangu karne ya 7.
Walikuwa wafanyabiashara na mabaharia hodari sana. Walijenga utajiri wao juu ya biashara ya ubao kutoka milima ya Lebanoni. Hasa miti ya aina ya seda (cedrus libani) ilitafutwa sana.
Baadaye waliunda koloni zao katika magharibi ya Mediteranea hadi Afrika ya Kaskazini na Hispania. Koloni yao mashuhuri ilikuwa Karthago.
[hariri] Mafanikio ya kihistoria ya Wafinisia
Wafinisia walianzisha mwandiko wa pekee uliokuwa chanzo cha alfabeti zote za Ulaya kupitia alfabeti ya Kigiriki.
Mabaharia Wafinisia walikuwa watu wa kwanza waliozunguka bara la Afrika kwa jahazi zao. Safari hii ilitokea mnamo mwaka 600 KK kwa niaba ya mfalme Necho II wa Misri aliyewaajiri kwa safari ile.