B

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz
Herufi B kwa mwandishi mbalimbali

B ni herufi ya pili katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Beta ya Kigiriki.

Maana za alama B[hariri | hariri chanzo]

Historia ya herufi B[hariri | hariri chanzo]

Kisemiti asilia
picha ya ramani ya nyumba
Bet ya Kifinisia
Beta ya Kigiriki B ya Kilatini
Proto-semitic house Phoenician beth Greek beta Roman B


Kama herufi nyingine za alfabeti ya Kigiriki beta imetoka katika alfabeti ya Wafinisia iliyokuwa alfabeti ya kwanza ya dunia. Wafinisia waliendeleza mwandiko wa kikabari wa kale uliokuwa mwandiko wa silabi na kuifanya alfabeti ya herufi moja-moja.

Faida ya alfabeti ni ya kwamba inahitaji alama chache kulingana na mwandiko wa silabi mwenye alama kwa kila silabi ya lugha fulani au mwandiko picha unaohitaji maelfu ya alama za picha.

Bet ya Wafinisia[hariri | hariri chanzo]

Wafinisia walichukua alama ya ramani ya nyumba wakairahisisha na kuiita kwa neno lao "bet" lenye maana ya "nyumba" lakini walisoma tu "b" yaani sauti ya kwanza katika neno hili. Hivyo walifanya picha ya nyumba kuwa herufi iliyo alama ya sauti "b". Herufi ilitazama upande wa kushoto pa kwa sababu mwendo wa kuandika ulikuwa kuanza upande wa kulia klwenmda kushoto jinsi ilivyo katika lugha za Kisemiti za Kiebrania na Kiarabu.

Kufuatana na kalamu tofauti (kama ni kuandika kwa kijiti kwenye udongo wa ufinyanzi au kwa wino kwenye karatasi) umbo la herufi likaandikwa kwa michirizo au zaidi kwa kona.

Beta ya Wagiriki[hariri | hariri chanzo]

Wagiriki walipokea alfabeti kutoka Wafinisia na pia jina la herufi hii. Wakabadilisha kidogo jina kuwa "beta" badala ya "bet". Lakini katika lugha yao hawakuelewa tena maana asilia iliyokuwa "nyumba". Kwao ilikuwa alama ya sauti tu.

Mwanzoni waliandika herufi kwa kutazama upande wa kushoto kama walivyofanya Wafinisia lakini katika karne za baadaye herufi iligeuzwa na kuandikwa mwishowe jinsi tunavyozoea leo.

B ya Kilatini cha Waroma wa Kale[hariri | hariri chanzo]

Waroma wa Kale walipokea alfabeti kutoka Wagiriki na kuibadilisha kwa mahitaji yao. Beta ikaitwa nao kwa sauti yake tu yaani "b" badala ya neno "beta".