V

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

V ni herufi ya 22 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni ipsilon katika alfabeti ya Kigiriki.

Maana za V[hariri | hariri chanzo]

Historia ya alama V[hariri | hariri chanzo]

Historia ya V ina asili za pamoja na U, W, Y na F. Historia hii ni ngumu kidogo kwa sababu alama ilipita katika alfabeti za lugha ambazo zilitumia hasa alama hii kwa sauti tofautitofauti. Kwa sababu hii matamshi yalibadilika kati ya lugha na lugha. Pia lugha mpya iliweza kuona haja ya kuunda alama mpya kwa sauti ya pekee.

Kisemiti asilia:
picha ya kingoe
Kifinisia:
Waw
Kigiriki:
ipsilon
Kietruski:
V
Kilatini:
V

Alama ya V kiasili ilimaanisha sauti za "v" na "u" kwa pamoja katika Kilatini cha Kale. Iliandikwa kama V na matamshi yake yalitegemea nafasi yake katika neno pia lahaja mbalimbali. Tofauti ilikubwaliwa tu wakati wa Kilatini Kipya katika karne ya 16 ambako wataalamu wa Ulaya walikubaliana kutumia alama yenye kona V kwa sauti ya konsonanti na alama isiyo na kona U kwa vokali.

Waroma walipokea alama hii kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na "waw" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya fimbo la kingoe au kiopoo. Wagiriki wa Kale walichukua alama hiyo na kuitumia kwa namna mbili: kwa umbo moja kama digamma (tazama F) na umbo la pili kama "ipsilon" bila kujali maana asilia ilitaja sauti kati ya "u" na "i".

Waitalia ya kwanza wakaendelea kutumia alama kwa aina ya "u" lakini pia "v" kama ilikuwa mwanzoni wa neno. Waroma walipokea vile.