I
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Alfabeti ya Kilatini | ||||||
|---|---|---|---|---|---|---|
| Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
| Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
| Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
| Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
| Ww | Xx | Yy | Zz | |||
I ni herufi ya 9 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Iota ya alfabeti ya Kigiriki.
[hariri] Maana za I
- Kwa magari I ni alama ya gari kutoka Italia.
- Katika kemia I ni alama ya elementi ya iodini.
- kati ya namba za Kiroma "I" ni alama ya namba 1
[hariri] Historia ya I
| Kifinisia Y (yad) |
Kigiriki Iota |
Kietruski I |
Kilatini I |
|---|---|---|---|
![]() |
![]() |
![]() |
Asili ya alama ni picha andishi iliyoonyesha mkono. Wafinisia walikuwa rahisihsa alama hiyo na kuiita kwa neno lao la mkono "yad" (au: yod). Wakaitumia kama alama ya sauti "y" na pia ya "i" ndefu. Wagiriki wakaipokea kama "Iota" na kurahisisha umbo lake zaidi hadi kuwa mstari tu. Wakaitumia kwa sauti ya "i".
Alama ikaendelea hivyo katika alfabeti za Waetruski na za Kilatini.
| Makala hiyo kuhusu "I" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu I kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |


