Turku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Turku

Turku ni mji wa Ufini mwenye wakazi 175.000. Iko kwenye pwani la kusini ya nchi mwambaoni wa Bahari ya Baltiki. Ilikuwa kitovu cha utamaduni wa Kiswidi katika Ufini lakini leo hii ni asilimia tano za wakazi pekee wanaosema Kiswidi. Kiswidi pamoja na Kifini ni lugha rasmi mjini.

Kuna pia Chuo Kikuu na askofu wa kanisa la kilutheri.