Nyeri
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Nyeri | |
| Mahali pa mji wa Nyeri katika Kenya | |
| Anwani ya kijiografia: 0°25′S 36°57′E / 0.417°S 36.95°E | |
| Nchi | |
|---|---|
| Mikoa | Mkoa wa Kati |
| Wilaya | Wilaya ya Nyeri |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 130 000 |
Nyeri ni mji wa Kenya ya kati takriban kilomita 100 kaskazini ya Nairobi mwenye wakazi 130,000 (2005). Iko mguuni wa safu ya Aberdares ikitazama mlima Kenya. Nyeri kuna makao makuu ya Mkoa wa Kati. Wakazi walio wengi ni Wakikuyu.
Nyeri imejulikana kimataifa kwa sababu ni mahali pa kuzikwa kwa Robert Baden-Powell anayekumbukwa kama mwanzilishaji wa harakati ya maskauti. Maskauti kutoka nchi mbalimbali za dunia hufika hapo mara kwa mara kwa kumheshimu mzee huyu.